Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa
Stanley Kolimba akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya leo
kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mjumbe wa
Halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) kutoka Ludewa Elizabeth Haule
........................................................................................................................................
CHAMA
cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kimempongeza
mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe kwa jitihada zake mbali mbali
za utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo hilo.
Pongezi
hizo zimetolewa na mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Stanley Kolimba
wakati akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya mjini
Ludewa leo
Kolimba
alisema kuwa mbunge utendaji kazi wa mbunge huyo umeendelea kuwa
chachu ya kimaendeleo katika jimbo hilo na kuwafanya wananchi
kuendelea kuwa na imani kubwa na CCM.
Alisema
mbunge huyo amekuwa mfano wa kuigwa katika kufanikisha utekelezaji wa
ilani ya CCM na kudai kuwa jitiihada kubwa zinazofanywa na
Filikunjombe zitasaidia kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na mapenzi
zaidi na CCM.
"Kweli mbunge wetu amekuwa ni mfano wa kweli
katika kufanikisha maendeleo ya jimbo letu na wilaya na hata majirani
wamekuwa wakipongeza utendaji kazi wake "
Katika
hatua nyingine CCM wilaya ya Ludewa kimewapa pore wananchi wa kata
ya Rupingu ambao wamepatwa na majanga ya mali zao mbali mbali yakiwemo
mazao kuharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo
mbali mbali hapa nchini.
"Mbali
ya mvua zinazoendelea kunyesha kusaidia kutupa neema ya mazao
yetu ila wenzetu wa Rupingu wamepatwa na majanga makubwa kutokana
na mvua hizo hivyo tunawapa pore kwa majanga haya yaliyowakuta."
Hata
hivyo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Ludewa
walipongeza jitihada za serikali ya awamu ya nne na jitihada za
mbunge wao katika suala zima la uboreshaji wa miundo mbinu katika
wilaya hiyo ya Ludewa kutokana na kuwa na miundo mbinu rafiki
isiyosumbua sana ukilinganisha na maeneo mengine.
Pia
waliiomba serikali kwa mwaka huu kuangalia uwezekano wa kutenga
bajeti kubwa zaidi ya fedha kwa ajili ya
ununuzi wa mahindi ya wananchi wote kutokana na kuwepo kwa dalili
nzuri zaidi ya wakulima katika wilaya hiyo kupata mazao zaidi
ukilinganisha na miaka iliyopita.
Kwani
walisema kutokana na jinsi ambavyo wakulima wengi walivyopata mazao
na kulima zaidi upo uwezekano wa wakulima kukosa soko la mazao
yao yote ama wenye fedha ndio watakaonufaika zaidi na soko hilo.
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe aliipongeza serikali ya Rais
Jakaya Kikwete kwa kuendelea kuboresha maisha ya wana Ludewa kwa
kufungua milango mbali mbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza
uboreshaji wa miundo mbinu ya wilaya hiyo.
Kwani
alisema mbali ya kuanza uboreshaji wa miundo mbinu hiyo tayari
wilaya ya Ludewa kwa mara ya kwanza toka nchi ipate uhuru wake
mwaka 1961 kwa kipindi hiki ambacho amekuwa mbunge wa jimbo hilo
tayari wananchi wa Ludewa wameanza kuona ujenzi wa barabara ya lami
ukianza pamoja na wananchi wa pembezoni ambao hawajafanikiwa kuwa na
umeme hivi sasa zoezi la kuwafikishia umeme limeanza.
0 comments:
Post a Comment