Timu
ya Taifa ya Malawi (Flames) inatarajiwa kuwasili nchini Mei 1 mwaka huu kwa
ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Mei 4 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Flames
yenye msafara wa 31 utakaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha
Mpira wa Miguu cha Malawi (FAM) utaingia Mbeya kwa usafiri wa barabara. Wachezaji
katika msafara huo ni 20.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya,
Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es
Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment