HOME »
» AFRICAN LYON WAALIKWA NCHIN ISPANIA KUFANYA MAZOEZI
KLABU
ya African Lyon inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara,
imepata mwaliko wa kwenda kuweka kambi mjini Barcelona nchini Hispania.
Taarifa
ya African Lyon iliyotumwa jana, imesema kwamba, mwaliko
huo wamepewa na kampuni ya Aspire Management, inayojishughulisha na
masuala ya michezo na ushauri wa kibiashara.
|
Tunakwenda Hispania; Mmiliki wa African Lyon, Rahim Kangezi 'Zamunda' amesema wamealikwa Barcelona |
Taarifa
hiyo imesema Lyon iliyoteremka kutoka Ligi Kuu misimu miwili iliyopita,
itafanya mazoezi katika viwanja vya Centre Esportiu na Aristides Mallol
ambavyo vimesifiwa ni vizuri na kwamba wachezaji watafanya mazoezi na
pia kuuona Uwanja wa FC Barcelona.
Taarifa
imesema kutoka viwanja vya mazoezi watakavyofanyia African Lyon
inachukua dakika mbili tu kufika Uwanja wa Camp Nou kwa kutembea na
kwamba Aspire wataiandalia mechi nne za kirafiki timu hiyo ya Tanzania.
“Pia wataandaliwa walimu wa Katalunya kutoka klabu kubwa kuja kuwafundisha wachezaji wa African Lyon,”imesema
taarifa ya timu hiyo inayomilikiwa na mjanja wa mjini Rahim Kangezi
‘Zamunda’ aliyeinunua kwa mfanyabiashara mkubwa na mwanasiasa Mohammed
‘Mo’ Dewji miaka minne iliyopita, ambaye naye aliinunua kwa
wafanyabiashara wadogo wadogo wa soko la Mbagala, enzi hizo ikiitwa
Mbagala Market.
Hata
hivyo, taarifa ya African Lyon, klabu iliyoibua wachezaji kadhaa nyota
nchini akiwemo Mbwana Samatta, ambaye sasa anacheza TP Mazembe ya DRC
haijasema watakwenda lini Katalunya na watakuwa huko kwa muda gani
.CHANZO
Na Dina Ismail, Dar es Salaam ktoka BIN ZUBERY
0 comments:
Post a Comment