Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
KOCHA wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi amesema kuwa kuwaamini vijana katika klabu kunahitaji kuwapa muda ili kufikia malengo.
Mwambusi amesema kuna mambo mawili yanatakiwa kuzingatiwa katika falsafa za mpira.
Mosi; falsafa ya mpira huwezi kuwajumuisha makocha wote kwasababu kila mtu ana falsafa yake.
Pili; kila klabu inakuwa na falsafa yake, hivyo inahitaji kocha atakayeiweza .
Mwambusi
aliendelea kufafanua kuwa klabu inapokuwa na falsafa yake, mfano
kutumia soka la vijana, lazima inakuwa na falsafa mbadala ili kama
itashindikana mpango A basi waende mpango B.
Kocha
huyo alisema si jambo la ajabu kuona timu inabadili mfumo wa soka lake
ndani ya msimu mmoja, lakini inategemeana na malengo ya klabu.
Akizungumzia
falsafa kwa Makocha, Mwambusi alisema kuna changamoto kubwa kwa walimu
wa kitanzania kwasababu huwa hawajiamini katika mifumo yao.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment