NONGA (WA KWANZA KULIA)AKIWA NA KIKOSI CHA MBEYA CITY. |
Mshabuliaji wa Mbeya City, Paul Nonga, amezikataa timu za Simba
na Yanga kwa kusema kuwa hafikirii kuondoka katika timu hiyo.
Nonga ameonyesha kiwango cha hali ya juu akiwa na timu hiyo ya mkoani
Mbeya ambayo imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu na amesema anataka
kuendelea kukaa kwenye timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatano, Nonga alifunguka kuwa,
hafikirii kuondoka Mbeya City kwa kuwa mtazamo wake ni kuhakikisha anaisaidia
timu hiyo ili iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu ujao.
“Kwa kweli sifikirii kuondoka Mbeya City kwani ndiyo timu iliyoniibua na nitabaki
hapahapa kwani ushindani tulioutoa kwenye ligi iliyoisha unatokana na
mshikamano tuliokuwa tukiuonyesha.
“Tunavyoishi katika kambi ya Mbeya City ni kama ndugu. Hakuna
tatizo lolote kwani tumezoea mazingira hayo ikiwa ni pamoja na uongozi kutupa
ushirikiano wa kutosha.
“Unadhani wote tukijazana Simba na Yanga nani ataijenga Mbeya
City? Kwani inaweza kubomoka msimu ujao
iwapo wachezaji wengi wataondoka na kuifanya timu ishuke kiwango, lengo letu ni
kutwaa ubingwa msimu ujao tukiwa na Mbeya City.
“Kiujumla ligi ilikuwa ngumu kwa kuwa kila timu tuliyokuwa
tukikutana nayo ilikuwa inatukamia na kutufanya tupoteze rekodi yetu ya
mzunguko wa kwanza ya kutofungwa, tulifanya makosa na wenzetu wakayatumia,
katika mzunguko wa kwanza walikuwa hawatujui,” alisema Nonga.
SOURCE: CHAMPIONI
0 comments:
Post a Comment