Tuesday, 29 April 2014

BAADHI YA WACHEZAJI WA MBEYA CITY WAFUNGUA MILANGO KWA AZAM, SIMBA, YANGA…

 
Picture 054 
Antony Matogolo mwenye jezi namba 16 mgongoni wakati wa mechi yao na Azam fc uwanja wa sokoine jijini Mbeya
Na Baraka Mpenja  , Dar es salaam
MMOJA wa kiungo  wa ulinzi wa Mbeya City fc, Antony Matogolo amebainisha kuwa kama timu yoyote itamhitaji na kumhakikishia maslahi mazuri anaweza kuondoka katika klabu yake hiyo iliyotikisa soka la Bongo msimu uliopita.
Akizungumza na mtandao huu, Matogolo amesema mpira ni maisha yake na inapotokea sehemu yenye maslahi mazuri zaidi hana budi kwenda.
“Kwa upande wangu mimi, soka ni maisha, halafu ni kazi. Hata wewe kwenye kazi yako inapotokea mtu mwingine mwenye maslahi mazuri anakuhitaji, haina budi kwenda sehemu unayoona itakusaidia zaidi”.
“Ni kweli naipenda timu yangu, naiamini, nawaamini viongozi wake na walimu wanaonifundisha, bado nina mkataba na Mbeya City fc”.
“Siwezi kusema nitaondoka kwa sasa hivi, lakini ikitokea, ninaweza kuangalia sehemu nyingine yenye maslahi mazuri”. Alisema Matogolo.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

0 comments: