DAVID
Moyes amepoteza kazi, hakuwa na ujanja na ilikuwa lazima iwe hivyo kwa kuwa
asingeweza kubadilisha mambo.
Ndani
ya miezi kumi, tayari Man United ilikuwa imepoteza mechi 11 za Ligi ya Mabingwa
Ulaya, hali iliyolazimisha kukatisha mkataba wake huo wa miaka sita.
Hapa
nyumbani imekuwa ni kawaida kabisa kuwaona Yanga na Simba wakiingia kwenye
mgogoro mkubwa na makocha wa kigeni na wazalendo kuhusiana na malipo yao.
Wanapokatisha
mkataba, kumlipa kocha inakuwa ni kazi ngumu na hadi kufikia mgogoro mkubwa.
Kama unakumbuka wakati ule Milovan Cirkovic alilazimika kuokolewa na Rahma Al
Kharoos ‘Malkia wa Nyuki’ kwa kuwa Simba ilishindwa kumlipa Sh milioni 36
zilizokuwa zinatakiwa kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.
Lakini
mkataba wa miaka sita umevunjwa kwa kitita cha pauni milioni 7 (zaidi ya Sh
bilioni 17.5), fedha ambazo zinaweza kuifanya Yanga, Simba au timu nyingine ya
Tanzania kuwa tajiri zaidi kama ikizikamata.
Moyes
amelipwa fedha hizo ambazo zinajumuisha mshahara wake wa mwezi, fedha ya
kuvunja mkataba pamoja na malipo ya usumbufu kutokana na uvunjani huo wa
mkataba.
Lakini
wakati wa uvunjani mkataba wake, kuna mambo kadhaa ya kiufundi yalifanyika
ambayo yanaashiria namna gani walioendelea katika michezo, mikataba yao
inavyokuwa na utaalamu.
Katika
mkataba wa Moyes, ilikuwa hivi. Kama angeifikisha timu katika nne bora na
kuweza kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi wakimfukuza ilikuwa ni lazima
alipwe kitita cha pauni milioni 9 (zaidi ya Sh bilioni 22.5).
Pamoja
na maji kuwafika shingoni, uongozi wa Man United uliendelea kufanya subira
katika jambo moja. Kuwa iwapo watafungwa mechi itakayothibitisha kuwa
hawatakuwa katika nne, maana yake wamekosa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya,
hapo watatoa pauni milioni 7 badala ya milioni 9.
Mkutano
wa mwisho waliofanya wamiliki wa Man United, Joe Glazer na wenzake ilikuwa ni
kujaribu kuokoa pauni hizo milioni 2 wakati Moyes anaondoka.
Mechi
dhidi ya Everton ndiyo ilikuwa na majibu, kama Man United wangepoteza maana
yake uhakika wasingefika nne bora na malengo ya uongozi kuokoa pauni milioni 2
ungekuwa umetimia.
Baada
ya Man United kufungwa mabao 2-0, viongozi wa Man United waliandaa mkutano mara
moja kumtaarifu kocha huyo kuhusiana na suala hilo na taarifa zikaanza kuvuja.
Huenda
wengi walishangazwa na namna ungozi wa Man United ulivyochelewa kumuondoa.
Lakini mambo mawili yalikuwa ya msingi zaidi kwao kuliko matakwa ya mashabiki.
Kwanza
kuangalia kama kungekuwa na mabadiliko ili Moyes aendelee, lakini kuhakikisha
kama imeshindikana, basi na pauni milioni 2 ambazo si haba, ziokolewe.
Hilo
ni moja la kujifunza kwa klabu za hapa nyumbani namna ambavyo mikataba
inaandaliwa kitaalamu na inakuwa imelenga mambo kadhaa na hata ukivunjika.
Zaidi unalenda kwenye kufanikiwa na kufeli na si ilimradi mkataba tu wa kazi,
hata wa kocha unaringana na wafanyakazi wote!
Kitu
cha pili cha kujifunza ni baada ya Moyes kumalizana na Man United na kuvunja
mkataba, hakuna ubishi ilikuwa ni lazima aondoke na kwenda kupumzika nje ya
England.
Moyes
alichagua Marekani, aliona ingekuwa sehemu nzuri ambayo angeweza kujipumzisha
kabla ya kuanza upya maisha ya mapambano.
Kwa
kuwa aliamua kwenda katika Mji wa Florida akiwa na mkewe na baada ya kulijua
hilo, bilionea Glazer alimpa Moyes ofa nyingine ya kufikia katika nyumba yake
ya kifahari iliyo mjini humo.
Pia
atapata huduma ya usafiri na usimamizi wa kutembezwa sehemu mbalimbali za jiji
hilo na wasaidizi wa Glazer.
Utaona
hivi, kocha akivunja mkataba au klabu kufanya hivyo. Basi uadui unatangulia na
ikiwezekana viongozi wa klabu hawataki hata kuzungumza na kocha kwa kuwa
anaonekana kama ni adui.
Glazer
ndiye anayepitisha uamuzi wa mwisho, lakini anaonyesha kiasi gani walivyoachana
kistaarabu na Moyes na hakuna tatizo lolote lililotokea.
Hivyo
mambo yako kitaalamu zaidi ndiyo maana wakati mashabiki wanaendelea kupiga
kelele. Moyes anakula ‘bata’ Marekani.
Na
Saleh Ally Kutoka saleh jembe blog
0 comments:
Post a Comment