MSHAMBULIAJI
wa klabu ya Monico, Radamel Falcao amesisitiza kuwa haionee wivu klabu yake ya
zamani ya Atletico Madrid kutokana na mafanikio yake msimu huu.
Nyota
huyo raia wa Colombia aliondoka Vicente Calderon majira ya kiangazi mwaka jana
na sasa kikosi cha Diego Simeone kimepata mafanikio bila yeye kwa kuongoza La Liga
na kufanikiwa kufika nusu fainali ya UEFA.
Hata hivyo,
mchezaji huyo wa zamani wa Porto amesena anafurahi kuona klabu yake ya zamani
inafanya vizuri na anataka kuona inafanikiwa zaidi.
“Sina
tatizo lolote na Atletico” . Amezungumza na Mundo
Deportivo.
“Najisikia
furaha kwa kile kinachotokea katika klabu. Nilijenga urafiki na kuwa na furaha
zaidi nilipokuwa pale”.
“Katika
maisha ya wachezaji kuna mabadiliko na huwezi kuwa na kila kitu.”
“Ninafuarahia
kwa wanachokifanya na nawatakia mafanikio makubwa zaidi”.
Falcao
kwa sasa yuko nje ya uwanja kutokana na
majeruhi, lakini anatarajia kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil
majira ya kiangazi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment