Kamati ya kutetea haki za
waandishi habari imelaani vikali kitendo cha serikali ya Ethiopia cha
kuwakamata waandishi habari 9 , wakielezea kama ni hatua mbaya zaidi
kuchukuliwa na serikali hiyo dhidi ya uhuru wa kujieleza nchini humo.
Mamlaka ya Addis Ababa imedai waandishi hao wa
magazeti na mitandao ya kijamii wanatumia nafasi zao kujaribu kuvuruga
amani nchini humo.Watetezi wa haki za binadamu wamemhimiza kuzungumzia swala hilo.
Serikali ya Ethiopia inaendeelea kukaza kamba na kukandamiza uhuru wa kujieleza kwa watu nchini humo hali ambayo imesababisha maandamano kwa wiki mbili zilizopita
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International, kukamatwa kwa wanablogu sita wiki jana ni sehemu ya mpango wa serikali kukandamiza upinzani.
0 comments:
Post a Comment