MSHAMBULIAJI hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa anaamini kuwa Chelsea hawatatumia mbinu yao ya kujilinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA hapo kesho uwanja wa Stamford Bridge.
Jose
Mourinho alitumia mbinu ya `Kupaki basi` katika mechi ya kwanza uwanja
wa Vicente Calderon na kulazimisha suluhu ya bila kufungana na alitumia
mbinu kama hiyo kuwafunga Liverpool mabao 2-0 jumapili iliyopita katika
mchezo wa ligi.
Hata
hivyo, Costa mwenye uraia wa Hispania anatarajia kuona Chelsea
ikishambulia zaidi katika mechi ya kesho jumatano kwa malengo ya kufika
fainali.
“Sina shaka, ni mchezo mkubwa, acha tufurahi na kuucheza”. Costa amewaambia waandishi wa habari.
“Itakuwa meci tofauti kwa wenyeji, watajitahidi kucheza kwa kushambulia zaidi”.
Atletico
msimu huu wana uchu wa kutwaa ubingwa wa La Liga tangu walipofanya
hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1996 na Costa ana ndoto ya kubeba kombe
Calderon.
“Ninataka
kushinda kombe la ligi na itakuwa furaha kubwa kufanya hivyo mbele ya
mashabiki wetu tutakapokutana na Malaga”. Aliongeza.
Atletico
Madrid katika mechi bili za mwisho watasafiri kuwafuata Levante na
mchezo wa kufungia msimu watakutana na Malaga nyumbani.
0 comments:
Post a Comment