MASHABIKI
wa Arsenal hivi karibuni watamuona tena uwanjani kiungo Abou Diaby
akiichezea timu yao, baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka kutokana na
maumivu ya goti.
Maumivu
ya mguu yalimuweka nje kwa muda huo mrefu mwanasoka huyo wa kimataifa
wa Ufaransa na sasa anapambana kwa mazoezi makali ya kujiweka fiti ili
kuanza kazi tena.
Mashabiki
hawana furaha na Diaby kwa sababu katika kipindi cha miaka minane ya
kuwa na klabu hiyo, ametumia muda mwingi zaidi kuwa nje ya kikosi
kutokana na majeruhi.
Lakini
picha alizopigwa hivi karibuni mjini Paris, Ufaransa zinamuonyesha
akifanya mazoezi makali ya kujiweka fiti baada ya kupona ili kurejea
uwanjani.
Mbio: Kiungo huyo wa Arsenal akikimbia kujiweka fiti
Mazoezi makali: Diaby akifanya mazoezi ya misuli
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Paris hajachezea kikosi cha kwanza
cha Arsenal tangu aumie goti katika mchezo dhidi ya Swansea Machi mwaka
jana.
Lakini
picha hizi zinaweza kumtuliza kocha Arsene Wenger na kuwajengea imani
mashabiki wa timu hiyo ya Uwanja wa Emirates, baada ya kumuona Diaby
akifanya mazoezi kamili ya nguvu kama kukimbia na kujenga misuli huku
akiwa mwenye tabasamu.
Kazi kazi: Diaby akijifua vikali
Diaby yuko karibu kurejea uwanjani tangu aumie goti Machi mwaka jana
Wenger amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo asubuhi kwamba hatamuharakisha Diaby kurejea uwanjani baada ya kupona.
Kiungo
huyo aliripotiwa kupata matatizo ya nyonga wakati akikichezea kikosi
cha vijana cha Arsenal chini ya umri wa miaka 21 dhidi ya Chelsea
katikati ya wiki ambayo itamfanya aukose mchezo wa Jumatatu dhidi ya
Newcastle.
"Diaby
alicheza kipinchi kimoja (kikosi cha U21),"alisema Wenger makao makuu
ya timu hiyo, Colney mjini London. "Bado ana mudea gani kurejea ni
vigumu kusema, lakini alipata matatizo kidogo ya nyonga baada ya mechi
hiyo,hivyo hatakuwepo Jumatatu," alisema Wenger.
Diaby cuts akimtoka Ruben Loftus-Cheek wa Chelsea katika mechi ya U21 Jumanne wiki hii
Diaby amekuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya mwaka tangu aumie
CHANZO BINZUBERY BLOG
0 comments:
Post a Comment