Afisa
Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Bw.Ernest Mamuya
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha kuwa kanuni na
taratibu za usafi wa mazingira zinazingatiwa na wananchi wote kwa
kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kujikinga na magonjwa
ya milipuko.
Afisa
Afya wa Manispaa ya Temeke Bw.Willium Muhemu akifafanua kwa waandishi
wa habari mafanikio yaliyofikiwa na Manispaa hiyo katika kuwaondoa
wafanyabiashara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi pamoja na
watu wote wanaochafua mazingira,Kulia ni Afisa Uhusiano wa Manispa hiyo
Bi. Joyce Nsumba.
(Picha zote na FRANK MVUNGI-maelezo)
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wananchi
wameaswa kuzingatia usafi wa mazingira kwa kuwa jukumu la kila
mwananchi kulinda na kutunza na kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira.
Hayo
yamesemwa na Afisa Afya wa Manispaa ya Temeke Bw. Willium Muhemu wakati
wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Bw.
Muhemu alisema manispaa hiyo imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha
kuwa kanuni za usafi, taratibu na sheria za usafi wa mazingira
zinazingatiwa na wadau wote wa mazingira ili kuepusha mlipuko wa
magonjwa.
“Moja
ya mikakati iliyowekwa na manispaa ya Temeke ni kuhakikisha kwamba
hakuna mtu anayefanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi ili kuzuia
uchafuzi wa mazingira na yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atachukuliwa
uchafuzi wa mazingira” Alisema Bw. Muhemu
Naye
Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Bw. Ernest Mamuya alisema kuwa ili
kuhakikisha kuwa manispaa hiyo inakuwa katika hali ya usafi wakati wote
wanao mpango mpango wa kuongeza magari ya kubeba taka , kuwa na dampo la
kudumu la kuhifadhia taka na kuhakikisha taka zinazolewa kwa wakati.
Akitoa
wito kwa wananchi Bw. Mamuya alisema kuwa wananchi wanapaswa kuzingatia
kanuni za usafi katika ngazi za familia ili kuunga mkono mpango wa
manispaa katika utunzani wa mazingira.
Maafisa
afya wa kata wanaendesha zoezi la ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kwa
kushirikiana na wajumbe wa kamati za afya za mitaa husika ili
kuhakikisha kuwa wananchi wanazingatia kanuni za usafi.
0 comments:
Post a Comment