KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALLY MWAKIBINYA (32) MKAZI WA MBUGANI
–KYELA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA KWENYE TAYA
LA KULIA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTO KIWIRA NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA ZAIRE MWAKIPESILE, MKAZI WA KIJIJI CHA IBANDA PAMOJA NA WENZAKE.
TUKIO
HILO LILMETOKEA MNAMO TAREHE 24.04.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI
HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUBELE, KATA YA BUSALE, TARAFA YA UNYAKYUSA,
WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. MAREHEMU AMBAYE ALIKUWA MKATA NYASI
ALIKAMATWA NA WATUHUMIWA TAREHE 23.04.2014 KWA TUHUMA ZA KUKATA NYASI
NA MTAMA KWENYE SHAMBA LA ZAIRE MWAKIPESILE NA KUDAI WANAMPELEKA
POLISI KISHA KUMUUA NJIANI. WATUHUMIWA WAMETOROKA KIJIJINI HAPO NA
JUHUDI ZA KUWATAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO
WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE MARA MOJA.
KATIKA MSAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO AMBAO NI 1. MICHAEL
MOSE (21) 2. NASSONO HASSAN (22) 3. KURWA IDDY (21) 4. HUSSEIN JUMANNE
(18) WOTE WAKAZI WA SOKOMATOLA NA 5. HASSAN MTANGA (22) MKAZI WA GHANA
KWA KOSA LA KUCHEZA KAMARI.
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 24.04.2014 MAJIRA YA SAA 13:45 MCHANA HUKO
ENEO LA SOKOMATOLA, KATA YA SOKOMATOLA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA
WA MBEYA. WATUHUMIWA WALIKAMATWA NA PESA TASLIMU KIASI CHA TSHS
21,250/=. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUCHEZA KAMARI KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA BADALA YAKE WATUMIE MUDA HUO KUFANYA SHUGHULI NYINGINE ZA
MAENDELEO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment