NAHODHA
wa Burundi, Didier Kavumbangu amesaini Mkataba wa miaka miwili na
mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC mchana wa
leo,
Kavumbangu
aliyemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam
FC baada ya kuona klabu yake haina mawasiliano naye licha ya kumaliza
Mkataba wake.
“Mimi
ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini
viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,”
amesema Kavumbangu akizungumza na mtandao huu baada ya kusaini Mkataba
huo ambao unamfanya alipwe vizuri kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.
|
Maisha mapya; Kavumbangu akitia dole gomba Mkataba wa Azam leo |
Pamoja
na hayo, Kavumbangu ameishukuru Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili
aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia kwenye kumbukumbu zake kwa
ameshinda nayo mataji.
Mshambuliaji
huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri
wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na
kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na
familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.
“Mimi
sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida
yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba
moja wa Azam,”amesema.
|
Tukutane Chamazi; Kavumbangu anahamisha virago vyake kutoka Jangwnai hadi Chamazi |
Kavumbangu
alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi
misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63
za mashindano yote, moja tu la penalti.
chanzo
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam Kutoka binzubery blog
0 comments:
Post a Comment