Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.
Watu
wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini
Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea
katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Bomu la pili lilipatikana katika gari hilo baada ya mlipuko huo na wataalamu wa mabomu waliliharibu.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao ambayo iliharibiwa vibaya kiasi cha kutoweza kutambulika.
Usalama umeimarishwa katika eneo hilo na polisi wanaendelea kufanya uchunguzi. Bosco
Mugendi ana kibanda cha kuuza vitu vidogovidogo karibu na lango la
kuingia kwenye kituo cha polisi cha Pangani kulikotokea mlipuko huo.
Alunukuliwa
akisema:"kile kilichonikuta katika kibanda changu ni nyama ya watu
iliyonirukia halafu mimi nikatoroka na kutoka nje."
Mtaalamu
wa maswala ya usalama jijini Nairobi, George Musamali, aliambia BBC
kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wakisindikiza gari kuelekea kituo hicho
cha polisi walikuwa kwenye gari la washukiwa ambalo lililipuka
baadaye.CHANZO BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment