Anelka, 35, aliposti video kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook jana Jumatano asubuhi ambapo alionekana kukataa kwamba alikuwa amesaini kujiunga na mabingwa Copa Libertadores .
Hata hivyo, raisi wa Atletico Mineiro, Alexandre Kalil, amepingana na Anelka, ambaye alimtangaza kumsaini tarehe 6 mwezi huu.
“Tutaelelezea kila kitu kuhusu uhamisho huu, kwa sababu tuna ushahidi wa kila kitu,” Kali aliwaambia waandishi wa habari.
“Tutakwenda FIFA. Itabidi atulipe fidia kwa kila kitu tulichotumia katika gharama za malazi na usafiri.”
Atletico Mineiro walitangaza wiki iliyopita kwamba wamefuta mpango wa kumsajili Anelka baada ya msjambuliaji huyo kushindwa kwenda kwa wakati Brazil.
0 comments:
Post a Comment