Monday, 28 April 2014

BRIAN UMONY: SING'OKI AZAM FC HATA KWA DAWA

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Uganda (Cranes) Brian Umony ameeleza kukoshwa kwake na weledi wa klabu yake ya Azam FC baada ya kumpa matunzo ambayo amedai ni ya kipekee katika kuhudumia wachezaji. Umony, nyota wa zamani wa KCC ya kwao Uganda na mfungaji wa goli la mwisho la Azam msimu wa 2013/14 alikaririwa na BBC Sport mwishoni mwa wiki akiumwagia sifa uongozi wa mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL) na kuweka wazi kwamba hakuwapa kupata matunzo mazuri kama hayo katika klabu zote alizopita tofauti na klabu hiyo ya Tanzania.
Azam raha' Brian Umony amesema anafurahia maisha Azam

"Azam ni klabu inayoendeshwa kwa misingi ya weledi, ina mipango inayoeleweka na wachezaji wazuri," alikaririwa Umony.
"Wananitunza vizuri hapa, Nimewahi kucheza sehemu nyingi, Afrika Kusini, USA, Vietnam na Uganda lakini hapa ni pa kipekee, Ninafurahia kutokana na kile ninachofanyiwa."
Umony ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni wanaokipiga katika klabu hiyo ya 'matajiri a Tanzania'. Wengine ni mapacha wa Ivory Coast Kipre Tchetche na Kipre Balou.
Klabu hiyo inayomilikiwa na bilionea mmiliki wa viwanda Said Salim Bakhresa, imeumaliza utawala wa Simba na Yanga - ambao wamwekuwa wakibadilishana ubingwa tangu 2000 - Mtibwa Sugar ilipolitwaa taji la ligi hiyo.
Umony alijiunga na Azam akitokea KCC FC January 2013 na amekuwa na mchango mkubwa katika timu hiyo ya 'wanalambalamba'. Kabla ya kutua Azam, mkali huyo wa kufumania nyavu alikuwa akikipiga Marekani, Afrika Kusini na Vietnam.
Na Renatus Mahima, Dar es Salaam

0 comments: