Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa
Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya
Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo
jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014). Kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde. (Picha na Martha Komba – Wizara
ya Katiba na Sheria).
Baadhi
ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo
(Jumatano, Aprili 30, 2014).
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo
katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo
(Alhamisi April 30, 2014) jijini Dar-es-salaam.
“Uwajibikaji
ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano
huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini
Dar-es-salaam.
Aidha,
Katibu Mkuu huyo aliwasihi watumishi wote wa Wizara yake kuungana na
wafanyakazi wote nchini na duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya
Wafanyakazi zinazofanyika kesho (Alhamisi, Mei 1, 2014).
Awali
akiongea katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo
aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao
za kazi.
“Tunapodai
maslahi ni lazima pia tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu
hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai
maslahi bora,” alisema Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na
viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya
Wizara hiyo.
Mkutano
huo, pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia
na kuridhia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao
wa fedha 2014/2015.
Na Martha Komba, Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment