Shirikisho
la ngimi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje Mh. Bernard Membe kwa hatua na jitihada alizozifanya za
kutafua na kufanikisha kambi ya mazoezi kwa Timu ya Taifa ya ngumi inayojiandaa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini Scotland.
Kwa
hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na maandalizi ya Timu
yetu ya Taifa kwa kuitafatia kambi ya mazoezi ya kimataifa Nchini
Uturuki na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika
hali duni bila ya kuwa na vifaa vya kisasa kulingana na mabadiliko ya
mchezo wa ngumi duniani.
Kwa
kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali katika
mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema
Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri
ya ushiriki waTanzania katika mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa
mara ya kwanza Tanzania ilishiriki mwaka 1972 na Tanzania kupata medali
ya kwanza ya kimataifa baada ya Tanzania kupata uhuru, iliyoletwa na
Bondia (LYTUS SIMBA) na baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta
medali ni kama wafuatao:
MICHAEL YOMBAYOMBA : (Dhahabu)
HAJI MATUMLA : (Fedha)
MAKOYE ISANGURA : (Shaba)
MWAMBEYA BAKARI : (Shaba)
WILLY ISSANGURA : (Shaba)
LUCAS MSOMBA : (Shaba)
Bado
BFT tunamuomba azidi kutusaidia vifaa zaidi hasa ulingo wa kisasa na
Computer inayotumika kuhesabia point za ushindi wakati wa mashindano
kwani Nchi zote duniani ndizo wanazozitumia na niagizo kutoka chama cha
ngumi cha dunia kwa wanachama wote lazima waitumie katika mashindano..
0 comments:
Post a Comment