Baadhi
ya viongozi wa ccm wakiwa katika picha ya pamoja sambambana picha za
waasisi wa muungano katika ngome ya mkwawa iliyoko kalenga
Na Denis Mlowe,Iringa
KATIKA
kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kimedhamiria kupitisha serikali mbili
katika bunge maalum la katiba, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wako
katika harakati za kuhamasisha wananchi kukubaliana serikali mbili
ambazo wamekuwa wakitumia mbio za pikipiki kueneza ujumbe huo kwa
kutumia jumuiya ya vijana wa chama hicho.
Akihutubia
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stand ya Mlandege
juzi,Kiongozi wa mbio za pikipiki kitaifa, Hassan Bamboko alisema lengo
za mbio hizo ni kufikisha ujumbe wa chama hicho kwa wananchi kuwa
serikali mbili ndizo zitakazopitishwa na chama hicho na kuwataka
wananchi kuuwanga mkono katika harakati hizo.
Alisema
licha ya kuhamasisha ujumbe wa serikali mbili ambao wananchi wengi
wamekuwa wakiukataa mbio hizo zinatumika kuadhimisha miaka 50 ya
Muungano wa Tanzania na Zanzibar ambao nao uko mashakani kutokana na
chama cha mapinduzi kuendelea kung’ang’ania serikali 2 badala ya tatu
ambazo ni chaguo la wengi.
“Mbio
hizi za pikipiki tunaenda nazo nchi nzima lengo nikuwaeleza wananchi
kuwa serikali mbili zinatosha wanaotaka tatu wanauchu wa madaraka na ni
mzigo kwa kweli na nawaomba muelewe hili kutokana na ni ya chama cha
mapinduzi kwa wananchi wake kuwa ni nzuri katika kulinda usalama wa
nchi” alisema Bamboko na kuongeza kuwa tuna miaka 50 tukiwa na Muungano
wa serikali mbili licha ya kuwa na kasoro zilikuwa chache na kuongezeka
zinaweza kurekebishwa na hakika serikali mbili zinatosha” alisisitiza.
Kwa
upande wake kiongozi mwingine wa mbio za pikipiki,Seki Kasuga
alisisitiza kuwa serikali mbili ndio mustakabali wa Watanzania katika
maisha ya mbele na wanaotaka kuugawa Muungano watafute kwanza udongo
uliochanganywa ili ugawanywe.
Naye Katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu akizungumzia kuhusu muundo wa Serikali
Tatu alisema Chadema wanatumiwa na magaidi wa nchi za nje kutaka serikali tatu ili kuwavuruga
wananchi.
Aliwataka
wananchi kumfikishia ujumbe Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe kuwa
serikali tatu haikubaliki kwa Watanzania hivyo wanajidanganya kwa kuwa
mwarubaini wa maendeleo ya Watanzania ni serikali mbili na sio tatu kama
zinazoshinikizwa na wapinzani.
Na Katibu wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa Halawi Haidari mwenyeji wa Zanzibar, alisema
Wazanzibar
wanautambua Muungano wa Serikali mbili hivyo hawawezi kutoka katika
Muungano kwa sababu Wazanzibar wapo huru kuishi popote katika ardhi ya
Tanzania
Alisema
kuwa muungano ukivunjika na kufikia hatua ya mgawanyiko watambue kuwa
hata Unguja na Pemba navyo vitagawanyika kwa sababu leo wamedai hati ya
Muungano wa Watanzania mwisho
watataka hati ya Unguja na Pemba lakini Wazazibar hawakubali msimamo wa serikali tatu.
Katika
mbio hizo vijana hao walikabidhi kwa kaimu mkuu wa wilaya ya Iringa,
Gerald Guninita picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Shekhe Abeid
Amani Karume pamoja na mabango mawili moja likiwa na ramani ya Tanzania
na lingine likiwa na ujumbe maaulum wa mbio hizo unaosema, miaka 50 ya
Muungano, “Dumisha Muungano vijana tutumie fursa zilizopo kwa maendeleo
yetu, Tanzania kwanza mengine baadae.
0 comments:
Post a Comment