Wednesday, 30 April 2014

AJALI YAUA MMOJA YAJERUHI 40 WILAYANI SUMBAWANGA

MTU mmoja amefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa baada ya ajali ya gari lililokuwa likitokea  katika kijiji cha Mkima Wilayani Sumbawanga kuacha njia na kupinduka na kutumbukia mtaroni.

Gari hilo aina ya Fuso lililokuwa limebeba  wachezaji wa mpira ambao walikuwa wakielekea  kijiji cha Mkima wakitokea Ilembo kwa ajili ya mechi ya kirafiki na kusababisha ajali baada ya kutumbukia mtaloni.

Kamanda wa polisi Mkoani Rukwa Jacob  Mwaruanda alisema mara baada ya gari hilo kupinduka lilisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Enani(18) aliyekuwa kapanda juu ya bomba na kusababisha kifo chake.

Kamanda Mwaruanda aliwataja baadhi ya majeruhi waliotibiwa na kuondoka kuwa ni Edmundy Nkalawa,Henrk Kaulule,Revokatus Malambika,Philibeth Zumba,Omary Jeusha,Joel Raphael na Lukas Kang’nga.

Wengine ni Daudi Sabino,Novakatus malambika,Seris Kisanzo,Aman Shaban,Crispin Nkalawa na Menady Msumbachika  ambao wote ni wakazi wa Lembo na  walitibiwa na kuondoka katika Hospital ya Mkoa.

Jeshi la polisi  lisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea dererva huyo alitoroka na upelelezi wa awali unafanyika na mara atakapo kamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayiomkabili.
 
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga

0 comments: