Monday, 28 April 2014

ASEC, ETOILE ZATINGA MAKUNDI AFRIKA

WANASOKA BORA WA MATOKEO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Jumamosi Aprili 26, 2014 Difaa Hassani El Jadida (Morocco) 2-1 Al-Ahly (Misri) (0-1)  Bayelsa Utd (Nigeria) 0-1 Sewe Sport (Ivory Coast) (0-1)  Jumapili Aprili 27, 2104 Nkana FC (Zambia) 1-1 Club Athletique Bizertin (Tunisia) (0-0)  Petro Atletico (Angola) 2-2 Coton Sport (Cameroon) (1-2)  Etoile du Sahel (Tunisia) 1-0 Horoya (Guinea) (0-0)  ASEC Mimosas (Ivory Coast) 1-0 Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) (1-2)  Medeama (Ghana) 2-0 (pk 4-5) AC Leopards (Kongo) (0-2)  Djoliba (Mali) 0-0 AS Real (Mali) (1-2)
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Afrika, ASEC Mimosas na Etoile du Sahel wamefuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushinda mechi zao mwishoni mwa wiki.
ASEC, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 1988, wamefuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2 dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, hivyo kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011.
Etoile, mabingwa wa mwaka 2006 walilazimika kusubiri hadi zikiwa zimesalia dakika sita Hamza Lahmar alipofunga bao pekee dhidi ya Horoya ya Guinea mjini Sousse, Tunisia na ‘Diables Rouges’ wamefuzu kwa ushindi wa jumla wa 1-0.
Mambo yalikuwa mabaya kwa ndugu zao, Club Athletic Bizertin ya Tunisia pia iliyotolewa na Nkana ya Zambia baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani, Derrick Mwanza akiwafungia wageni bao muhimu la ugenini dakika ya 79, baada ya Khaderi Med Arbi kutangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 20.

Kipute kikali: ASEC imefuzu kwa mara ya kwanza hatua ya makundi michuano ya Afrika tangu mwaka 2001
Nkana, iliyolazimishwa sare ya 0-0 katika mchezo wa nyumbani, inakuwa timu pekee ya Kusini mwa Afrika kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo. Mabingwa wa Cameroon, Coton Sport wamepata sare ya 2-2 mjini Luanda, Angola dhidi ya wenyeji Petro Atletico na kufuzu pia. Timu hiyo ya Garoua ililazimika kusawazisha mabao mara mbili na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-3 Wawakilishi wa Ghana, Medeama, wametolewa na AC Leopards ya Kongo kwa penalti, kipa Muntari Tagoe na Hans Kwofie walifunga dakika za mwishoni kuumaliza mchezo kwa sare mjini Sekondi na kuhamia kwenye penalti, ambako Wakongo walishinda 5-4. Mjini Bamako, Djoliba imetolewa na AS Real zote za Mali kwa jumla ya mabao 2-1. Mapema Jumamosi vigogo wa Misri, Al Ahly na Sewe Sport ya Ivory Coast zilitangulia kufuzu hatua hiyo. Droo ya ligi ndogo ya makundi ya michuano hiyo inatarajiwa kupangwa kesho asubuhi makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.

0 comments: