MAAFANDE
wa Tanzania Prisons `Wajelajela` wanasubiri kwa hamu kubwa ripoti ya
kocha wao, David Mwamwaja ili waanze kuandaa mikakati mapema kuelekea
msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Katika
mahojiano maalum na Mtandao huu, Katibu mkuu wa Prisons, Inspekta
Sadick Jumbe amesema misimu miwili mfufulizo wamenusurika kushuka
daraja, hivyo malengo yao ni kusajili wachezaji wazuri ili msimu ujao
washeka nafasi tano za juu.
“Sisi
ni viongozi na tuna majukumu yetu. Tumeona makosa yetu, lakini
inapofika mambo ya ufundi, Mwamwaja ndiye mwenye majukumu”.
“Tuna imani na kocha huyo mwenye historia kubwa katika soka. Anaandika ripoti yake ambayo tutaipata ndani ya wiki moja ijayo”.
“Kwa
kufuata mapendekezo yake, sisi viongozi tutatekeleza kila alichokiona na
kumshauri kwa yetu machache tuliyoyaona kwa nafasi ya viongozi”.
Alisema Jumbe.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment