Monday, 28 April 2014

IMANI ZA KISHIRIKINA ZINAKWAMISHA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA

 



Na Amon Mtega Songea
BAADHI ya wananchi katika kata ya Liganga, Songea vijijini mkoani Ruvuma wamekuwa na Imani potofu wauguapo Maralia hivyo elimu ya ugonjwa huo bado ni changamoto vijjini.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Ernest Haule wakati akizungumza katika Siku ya Maralia iliyoandaliwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Shamba la Kahawa la Kampuni ya Aviv Tanzania LTD.
'Elimu ya Maralia hapa ni changamoto na kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuandaa siku hii ya Maralia kwa kushirikiana na Kampuni ya Aviv katika Kata hii ya Liganga,'anasema Mtendaji huyo na kuongeza kuwa Maralia ni ugonjwa wa kawaida hivyo wananchi wanapaswa wanapojisikia dalili za Maralia kuwahi kupima na kupatiwa matibabu badala ya kuamini ushirikina.
Kwa upande wake Msimamizi wa Shamba hilo la Kahawa kutoka Kampuni ya Aviv Tanzania LTD, Amilt Kumar amesema kuwa wameandaa siku hiyo ambayo huadhimishwa kila Aprili 25 kwa wafanyakazi 1000 kushindwa kufanya Shughuli zao sawasawa.

0 comments: