Na Gladness Mushi, Arusha
MJUMBE wa kamati kuu ya CCM, taifa,
Abdalah Mihewa, amemshangaa ,Katibu mkuu wa Chadema, Dakta Wilbroad
Slaa, kwa kubeza maendeleo yaliyopatikana jimboni Karatu.
Mihewa
amesema hayo jana kwenye ofisi ya CCM, wilaya ya Karatu, baada ya
kupokea salaam za Chama kutoka kwa katibu wa Chama wilatya ya Karastum,
Elly Minja, na kusema kuwa,kiongozi huyo hana shukurani.
Mihewa
ambae pia ni katibu wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, aliyekuwa ziarani
wilayani Ngorongoro, kusimamia uchaguzi wa viongozi wa baraza la Umoja
wa vijana mkoa wa Arusha, amesema serikali ya CCM, imefanya mengi
jimboni Karatu ikiwemo kujenga bara bara ya Lami kutoka Arusha hadi
Lango kuu la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, pia serikali imetekeleza
mradi mkubwa wa maji kwa wananchi wa Karatu jambo ambalo ni ukombozi
mkubwa lakini Salaa bado anabeza kuwa hakuna kilichofanyika .
Amesema
kuwa Serikali ya CCM, inahudumia watanzania wote bila kujali itikadi
hata kama majimbo yanaongozwa na wapinzanilazima wananchi waliopo
watapata huduma bila ya ubaguzi wala upendekleo.
Serikali
ya CCM,inaboresha miundo mbinu nchini kote bila kujalilakini leo mtu
mzima anaponda na kubeza huyo ana matatizo ya akili hata angelikuwa ni
kipofu basi angelipapasa aone nini kilichofanywa na serikali ya
CCM,jimboni humona sio kubeza
Akawataka viongozi na wananchi kuimarisha mshikamanona kujipanga kulikomboa jimbo hilo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi .
Awali Katibu
wa CCM, Wilaya ya Karatu, Elly Minja, katika salam zake amesema
wananchi wilayani Karatu wamechoshwa na miaka 17 ya Chadema tangia
kuchukua jimbbo hilo wamekwama kimaendeleo.
Amesem,a
wananchi jimboni humo wanadai wameschoshwa na maneno bila vitendo sasa
wanajiandaa kuking’oa chama cha Chadema, ili waweze kupata maendeleo
kutoka Chama cha mapinduzi ambacho serikali yake inawapatia huduma
mbalimbali ikiwemo mnradi mkubwa wa maji ambao limekuwa ni tatizo kubwa
na la kudumu.
Amesem,a
wananchi pia wamechoshwa kufanywa ngome ya Chadema,na sasa wameahidi
katika uchaguzi mkuu ujao kukiondoa chama hicho cha Chadema..
0 comments:
Post a Comment