>>WAZIRI MKUU UINGEREZA AINGILIA KATI ILI BAA ZIWE WAZI!
WAZIRI MKUU wa Uingereza, David Cameron, ametaka ifikiriwe upya ili kuruhusu Mabaa kubaki
wazi
Usiku wa Manane ili kuruhusu Watu kutazama Fainali za Kombe la Dunia
zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12 baada ya Mawaziri kupinga
Mabaa hayo kuwa wazi kwa Mechi za England.
Wamiliki Pabu hizo waliomba muda wao wa
kuwa wazi uongezwe lakini Wizara ya Mambo ya Ndani ilipinga ombi hilo
lakini sasa kuna taarifa toka Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa ruhusa
itatolewa.
KOMBE LA DUNIA-BRAZIL 2014
England=Kundi D:
RATIBA:
-Juni 14: v Italy
-Juni 19: v Uruguay
-Juni 24: v Costa Rica
England, ambao wako Kundi C kwenye
Fainali za Kombe la Dunia, wataanza Mechi zao Juni 14 kwa kucheza na
Italy Saa 5 Usiku kwa Saa za Uingereza, ikiwa ni Saa 7 Usiku Saa za
Bongo.
Katika Mechi zao nyingine mbili za Kundi
C, England watacheza na Uruguay kuanzia Saa 2 Usiku kwa Saa za
Uingereza, ikiwa ni Saa 4 Usiku Saa za Bongo na kufuatia Costa Rica
watakayocheza Saa 11 Jioni, Saa za Uingereza, ambayo ni Saa 1 Usiku kwa
Bongo.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia za
Mwaka 2010 zilizochezwa huko Afrika Kusini, zaidi ya Watu Milioni 4
waliitazama Mechi ya ufunguzi ya England wakiwa kwenye Pabu huko
Uingereza.
0 comments:
Post a Comment