KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah
Kibadeni, amebariki kuondoka kwa kiungo, Amri Kiemba, aliyejiunga na Yanga
akiwasihi viongozi wa klabu hiyo wamwache akatafute masilahi zaidi kwa ajili ya
maisha yake.
Kauli
ya Kibaedeni, nyota wa zamani wa Majimaji ya Songea, Simba na Taifa Stars,
imekuja baada ya kiungo huyo aliyeifungia Stars bao dhidi ya Morocco mwishoni
mwa wiki ilipolala 2-1, kuripotiwa kuwa ametua Yanga kwa dau la shilingi mil.
35.
Kibadeni
aliyejiunga na Simba siku chache zilizopita akitokea Kagera Sugar, alisema jana
kuwa mpira ndio kazi ya kiungo huyo, hivyo kwa upande wake hatakuwa kikwazo na
anamruhusu kwa mikono miwili kujiunga na Yanga kwa sababu anatafuta masilahi
kwa ajili ya maisha yake.
“Kwa
vile wachezaji wengi wa Tanzania soka ndiyo ajira yao, nashindwa kumzuia kwa
vile kila mchezaji mwenye malengo amekuwa akipambana kufikia kiwango fulani
katika maisha.
“Mimi
inakuwa vigumu kumzuia Kiemba asiende Yanga kwa kuwa mpira ni kazi yake
japokuwa ni pengo kubwa kwa Simba, namtakia kila la heri aweze kufanikiwa,”
alisema Kibadeni.
Kibadeni
alikwenda mbali zaidi na kusema kutokana na uwezo wa Kiemba dimbani, alitamani
sana kuwa naye kwenye kikosi cha Simba, lakini imekuwa vigumu hivyo, anaomba
Mungu apate mbadala atakaye fanya kazi kama kiungo huyo.
Kiemba
ambaye ni miongoni mwa viungo mahiri wa sasa nchini, kabla ya kutua Simba
aliwahi kuichezea Yanga kwa misimu kadhaa aliyokuwa amejiunga nayo akitokea
Kagera Sugar ya Kagera, misimu kadhaa iliyopita.
Kiemba
anakuwa mchezaji wa pili kutua Yanga akitokea Simba, amesaini mkataba wa miaka
miwili huku kukiwa na habari kuwa atakuwa akilipwa mshahara wa sh milioni mbili
kwa mwezi. Kabla ya Kiemba, Yanga ilifanikiwa kumsajili Mrisho Ngasa.
Alipotafutwa
Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, kuhusu Kiemba, alisema anavyojua yeye
ni kwamba mchezaji pekee kutoka Simba hadi sasa ni Ngasa na kama ni kweli
wamemsajili Kiemba, watu wasubiri muda utakapofika.
0 comments:
Post a Comment