SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amewatuhumu
wabunge wenzake kwa ubinafsi unaowasababisha wasiunde mtandao wa pamoja
kusimamia masuala yanayogusa maslahi ya nchi.
Makinda
alitoa tuhuma hizo jana mjini hapa wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa
mwaka wa Chama cha Mabunge Afrika Wanaopambana na Rushwa (APNAC).
Alisema
hivi sasa kila mbunge anaibuka na hoja yake bila kuwashirikisha wenzake ili
aonekane ndiye mwanzilishi wa jambo fulani.
Kiongozi
huyo alitoa tuhuma hizo alipokuwa akijibu malalamiko ya baadhi ya wadau
wakiwemo wabunge, kuhusu usiri wa mikataba ambayo walitaka iwekwe wazi ili
wananchi waione na kuisoma.
Alisema
mikataba hiyo inapatikana kwa wabunge kupitia ofisi yake, lakini baadhi yao
wamekuwa wakienda kuipitia kila mmoja kwa wakati wake badala ya kuunda mtandao
wa kusaidiana na kuibana serikali pale wanapotaka kuleta hoja bungeni.
“Tatizo
ninaloliona kwa Bunge langu la sasa, siku hizi ile ‘net working’ (mtandao) kati
ya wabunge haipo. Maana haitoshi wewe peke yako unakwenda kusoma mkataba halafu
ukaibua hoja. Utakuwa peke yako.
“Kila
siku nawaambia kuwa nimekuwa mbunge tangu mwaka 1975, tulikuwa na mtandao wetu
wa kuipinga serikali. Mnakaa mnajadiliana hoja kwa nguvu kabisa na ikija
bungeni hakuna namna serikali inaweza kushinda,” alisema.
Aliongeza
kuwa hata wakati wa kujadili miswada ya sheria, kuna baadhi ya wabunge wanakaa
peke yao na kuandaa mabadiliko kisha wanayapeleka kwake ikiwa imebakia nusu saa
ambapo ni kinyume na kanuni.
Alisema
kuwa anapoyakataa mabadiliko hayo, wabunge husika hukimbilia kwenye vyombo vya
habari kulalamika kuwa anapendelea wakati wakijua walikosea kuwasilisha
mabadiliko yao.
“Mngekuwa
na mtandao mngekuwa mnakuja bungeni mmekamilika. Lakini kila mtu anasimama
anazungumza masuala yake ya vyama badala ya matatizo ya nchi ili aonekane kwenye
TV kuwa ndiye muasisi wa hoja hiyo,” alisema.
Alisema
ili wabunge waweze kupambana na rushwa, lazima wajiwekee mfumo wa maadili kwa
kujitazama wao kabla ya kuwanyooshea vidole wengine.
Chanzo jaizmelaleo bolg
0 comments:
Post a Comment