Thursday, 13 June 2013

MAHAKAMA KUU KANDA YA MBEYA YATUPILIA MBALI KESI YA UBAKAJI

 


Mshitakiwa Isambi Mwazembe akiwa haamini kama kesi yake imeisha 

Mshitakiwa Isambi Mwazembe akiwa mwenye Furaha baada ya kesi yake kwisha 


Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imemwachia huru Mshitakiwa wa kosa la ubakaji aliyekuwa amehukumiwa kutumikia kifungo cha miak 30 na Mahakama ya Wilaya.

Mtuhumiwa huyo Isambi Mwazembe (29) alidaiwa kutenda kosa hilo Mwaka 2003 ambapo baada ya kukutwa na hatia alihukumiwa kifungo hicho kasha kutumikia kifungo miaka minne kabla ya Mahakama kuu kumwachia huru baada ya kukata rufaa.

Akipitia rufaa iliyoletwa mahakamani hapo Jaji Atuganile Ngwala amesema sababu kubw iliyosababisha atengue kifungo hicho ni kipengele kilichotumiwa na mahakama ya chini kuwa hakikufanywa kisheria.

Amesema kipengele kilichotumika ni kwamba Mahakama hiyo ilipokea PF 3 kutoka kwa mhanga wa kosa ilo badala ya kupokea kutoka kwa Daktari  aliyemfayia vipimo kama kielelezo.

Pia amesema katika maelezo ya daktari yanadai binti huyo kubakwa baada ya kukutwa na michubuko na damu sehemu zake za siri licha ya kumkuta na Bikra kitendo lichodai kuwa sentensi hiyo haikuwa na uhkika.  

Chanzo na MBEYA YETU


0 comments: