Thursday, 20 June 2013

WATU 48 WAUAWA ZAMFARN NIGERIA

 
Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki wamewaua watu 48 katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja katika jimbo la Zamfara.
Watu hao waliwasili kabla ya macheo wakiendesha pikipiki.
Baadaye walikwea mlima uliokuwa karibu na kijiji hicho na kuanza kuwafyatulia watu risasi kiholela nyumba hadi nyumba.
Shambulizi hilo linasemekana kuhusishwa na mgogoro kuhusu wizi wa Ng'ombe katika jimbo la Kaskazini . Kulikuwa na mashambulizi kama haya mwaka jana.
Jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu pamoja na kuwa inazalisha mafuta, pia linakabiliwa na tatizo la makundi ya wapiganaji wa kiisilamu wanaofanya mashambulizi mara kwa mara.
Hata hivyo, ghasia za hivi karibuni haziaminiki kuwa na uhusiano wowote na harakati za wapiganaji wa kiisilamu wa Boko Haram.
Miongoni mwa waliouawa ni Chifu, Imamu na kiongozi wa kundi la vijana wanaotoa ulinzi.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa wavamizi waliwasili katika eneo la Kizara kabla ya macheo wakiwa kwenye pikipiki na kuwa walijipanga kwa mashambulizi kabla ya kuanza kuwaua wanavijiji.
 

0 comments: