Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema kuwa haiwezi
kuziruhusu timu za Tanzania kushiriki katika mashindano ya Klabu Bingwa
Afrika
Mashariki na Kati kutokana na hali ya usalama ya Darfur.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Amos Makalla baada ya gazeti hili
kutaka kujua hatima ya timu za ushiriki wa timu za Tanzania katika
mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
“Nipo
kwenye kikao cha baraza la mawaziri, hata hivyo hatuwezi kuziruhusu
timu zetu kwenda eneo ambao si salama, pamoja na kusubiri taarifa rasmi
kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,” alisema Makalla.
Kauli
hiyo inaifanya timu za Yanga kupoteza ubingwa wake, huku Simba na
Super Falcon kuachana na mashindano hayo kutokana na sababu hiyo
muhimu. Timu hizo pamoja na Shirikisho la Soka nchini, TFF lilikuwa
linasubiri taarifa rasmi kutoka serikalini.
Awali,
Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini, TFF, Leodegar Tenga alisema
kuwa wao hawana taarifa zozote kuhusiana na uamuzi wa Serikali zaidi
ya kauli yao ya kwanza.
“Sina taarifa, labda wewe una taarifa rasmi kuhusiana na uamuzi wowote kuhusiana na hatima ya timu za Tanzania katika mashindano hayo,” alisema Tenga ambaye pia ni Rais wa Cecafa.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema kuwa
hali ya usalama wa Darfur si nzuri na kuiomba TFF ifikirie upya uamuzi
wa upeleka timu Darfur kwani kuna ushahidi kuwa hali ya usalama si
nzuri.
“Tuna
ushahidi kuwa hali ya Darfur siyo nzuri kiusalama, tumewaandikia TFF
kuwaeleza hayo na kuwaomba wafikirie upya ushiriki wa Tanzania katika
mashindano hayo,” alisema Membe.
SOURCE: MWANANCHI.COM
0 comments:
Post a Comment