Monday, 10 June 2013

MAAFISA 32 WA WANYAMA PORI WASIMAMISHWA KWA TUHUMA ZA UJANGILI NCHINI KENYA

Kiasi cha maafisa waandamizi 32 wa Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS) wamesimamishwa kazi ili kuruhusu uchunguzi ufanyike kutokana na kuongezeka kwa shughuli za ujangili katika maeneo yao, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti hapo Jumamosi (tarehe 8 Juni).

Maafisa hao waliosimamishwa ni pamoja na wale wenye dhamana ya mbuga nchini kote pamoja na maafisa kadhaa katika makao makuu ya KWS, alisema Mkurugenzi wa KWS William Kibet Kiprono.

Maafisa wameshukiwa kwa kushirikiana na majangili na wataondolewa moja kwa moja na kuchukuliwa hatua za kisheria iwapo uchunguzi utathibitisha shutuma hizo, alisema. --

Source: via SABAHIonline

0 comments: