MNAMO TAREHE 19.06.2013 MAJIRA YA SAA
13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUMBILA KATA YA RUANDA WILAYA YA MBOZI MKOA WA
MBEYA. RAJABU S/O WILSON MWASHITETE, MIAKA 25, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI
CHA LUMBILA ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI WALIOKUWA KATIKA MSAKO
DHIDI YA WAHALIFU/WAPORAJI KATIKA ENEO LA MLIMA SENJELE.
CHANZO NI BAADA YA ASKARI POLISI
WAKIWA KATIKA OPERESHENI ENEO HILO KUZINGIRWA NA KUNDI LA WANANCHI ZAIDI YA 150
WA KIJIJI HICHO WAKIWA NA SILAHA ZA JADI MAPANGA, MARUNGU, SHOKA NA MAWE
WAKIWAZUIA ASKARI HAO KUKAMATA WAHALIFU NA KUANZA KUFANYA VURUGU BAADA YA KUWA
WAMEKAMATA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI AMBAYO NI MAFUTA AINA YA DIESEL
MADUMU ZAIDI YA 100.
HATA HIVYO KUFUATANA NA VURUGU
ZILIZOJITOKEZA WALIFANIKIWA KUCHUKUA MADUMU MACHACHE AMBAYO NI MADUMU MATATU
YENYE UJAZO WA LITA 60, MADUMU MAWILI YENYE UJAZO WA LITA 20 NA MADUMU NANE
LITA 30 HIVYO UVAMIZI HUO WA WANANCHI NDIO ULIOWAFANYA ASKARI POLISI WASHINDWE
KUCHUKUA VIELELEZO VYOTE.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI.
AIDHA KATIKA TUKIO HILI CHARLES
S/O JOSE MWAWALO,MIAKA 27,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA LUMBILA
ALIJERUHIWA KWA KUPATA MICHUBUKO TUMBONI AMBAPO UCHUNGUZI UNAFANYWA KUBAINI NI
KITU GANI KILICHOMJERUHI.
PIA WANANCHI WALIFUNGA BARABARA KUU
YA MBEYA/TUNDUMA KWA KUWEKA MAWE NA MAGOGO NA KUSABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA
MAGARI BARABARANI.
HALI ILIKUWA SHWARI BAADA YA KAMANDA
WA POLISI KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI KUFIKA ENEO LA TUKIO NA
KUZUNGUMZA NA WANANCHI PAMOJA NA VIONGOZI WA ENEO HILO KISHA KUFUNGUA BARABARA
.
ASKARI POLISI WANNE WALIJERUHIWA
KATIKA TUKIO HILO KATI YAO WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA ASKARI
MMOJA AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU ZAIDI .
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA
YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA BADALA YAKE KUWA NA
UTAMADUNI WA KUTATUA KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO KWA
KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA. AIDHA ANAWATAARIFU WALE WOTE WALIOWAHI
KUIBIWA/KUPORWA MALI MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA WAJITOKEZE POLISI KWA AJILI YA
HATUA ZINAZOSTAHILI.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
|
0 comments:
Post a Comment