Wednesday, 12 June 2013

MH. ABBASS KANDORO AMALIZA MGOGORO KATI YA MADIWANI NA MKURUGENZI KYELA‏

 

Serikali Mkoani Mbeya imeumaliza mgogoro uliokuwepo baina ya Madiwani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbaralali, Abdallah Mfaume, uliodumu kwa miezi kadhaa. 
Mgogoro huo ulitokana na tuhuma za Madiwani hao dhidi ya Mkurugenzi kwamba anakiuka maadili ya Utumishi wa Umma ikiwemo kupindisha maamuzi mbalimbali ya Baraza la Madiwani kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Kutokana na tuhuma hizo Madiwani hao kupitia kikao cha Baraza lao Aprili 11 mwaka huu walitoa tamko la kuitaka Serikali kumfukuza kazi Mkurugenzi huyo hatua iliyozidisha mvutano baina ya pande hizo.

Lengo hilo halikuweza kufanikiwa kutokana na suala hilo kuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, ambaye kwa mujibu wa kanuni za Utumishi wa Umma hana mamlaka ya kumsimamisha kazi bali mwenye uwezo huo ni Waziri mwenye dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliunda tume ya Watu Watatu kuchunguza tuhuma hizo baada ya Mkuu huyo kupata taarifa ya Madiwani hao na kusikiliza utetezi wa Mkurugenzi huyo ili kutoa tarifa ya kina kwa Waziri wa TAMISEMI mwenye jukumu la kuamua hatma ya Mkurugenzi huyo. 

 Akiwasilisha kauli ya Baraza la Madiwani hao, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Gabriel Kipita, alidai licha ya tuhuma wanazimtuhumu Mkurugenzi huyo lakini jambo lililochochea mgogoro huyo na kuharibu muhusiano baina ya pande hizo ni kitendo cha Mfaume kukosa mahusiano mema na baadhi ya watendaji wakiwemo Madiwani hao.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa Kandoro, aliwataka Madiwani hao kuwa watulivu na kusubiri uamuzi wa Serikali kuhusu suala hilo kwa maelezo kuwa walichokiamua ni mapendekezo ambayo yanafanyiwa kazi lakini hawama mamlaka ya kufukuza kazi Mkurugenzi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.

“Ndugu zangu Madiwani, mapendekezo yenu yanafanyiwa kazi, kimsingi hamna mamlaka ya kumfukuza kazi Mkurugenzi, hata mimi sina mamlaka hayo, mwenye mamlaka ya nidhamu dhidi ya Mkurugenzi huyu ni Waziri wa TAMISEMI, tumwachie afanye kazi yake tusiingilie utaratibu, naomba muwe na subira wakati Serikali ikilishughulikia suala hili.” alisema Kandoro.

Kuhusu ombi la Madiwani hao la kutaka Mkurugenzi huyo asimamishwe kazi wakati suala lake likishughulikiwa, Kandoro alisema suala hilo haliwezekani kwani kinachomkabili ni tuhuma ambazo bado hazijathibitishwa.

Naye Diwani wa kata ya Ngonga, Kileo Kamomonga, alisema bila ya Kandoro kuzikutanisha pande hizo mgogoro huo usingemalizika kirahisi kutokana na mgawanyiko mkubwa uliokuwepo baina ya Madiwani na Watendaji wa halmashauri hiyo hasa Mkurugenzi huyo.

0 comments: