Hali
ya rais wa zamani wa Afrika kusini,Nelson
Mandela ,imeendelea kuwa mbaya katika hospitalini mjini
Pretoria ikiwa ni siku ya pili leo tangu Rais
Jacob Zuma alipomtembelea na kusema shujaa
huyo wa kupambana na ubaguzi wa rangi
alikuwa amelala.
Rais Jacob Zuma amewaambia waandishi habari wapatao 60 kuwa madaktari wanafanya kila linalowezekana kurejesha hali yake kuwa bora wakati anatimiza siku ya 17 hospiatalini. Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria mapema mwezi huu akisumbuliwa na maambukizi katika mapafu. Ni mara ya nne kwa kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94 kulazwa hospitali tangu Desemba mwaka jana akipatiwa matibabu.
Zuma pia amesema kuwa madaktari wamesema hali ya rais huyo wa zamani imekuwa mbaya katika muda wa saa 24 zilizopita. Mandela alifungwa jela miaka 27 wakati wa utawala wa kibaguzi . Alichukua nafasi ya juu katika kuibadilisha nchi hiyo kuwa ya kidemokrasia , na amekuwa rais wa kwanza wa Afrika kusini mwenye asili ya nchi hiyo mwaka 1994.
0 comments:
Post a Comment