Wafungwa wanne wamenyongwa
kusini mwa Nigeria, katika kile maafisa wanasema kuwa hukumu ya kwanza
ya kunyongwa kutekelezwa kwa miaka saba.
Kamishna wa haki katika jimbo la Edo, Henry
Idahagbon, aliambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao walinyongwa
baada ya kuhukumiwa kifo kwa makosa ya wizi wa mabavu na mauaji.
Zaidi ya wafungwa 1,000 nchini Nigeria wanaaminika kuhukumiwa kifo .
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa Rais
Goodluck Jonathan hivi karibuni aliwataka magavana wa majimbo kutia
saini vibali vya hukumu ya kifo katika jitihada za serikali kupunguza
visa vya uhalifu.
Bwana Idahagbon alisema kuwa wananume wanne
walinyongwa katika gereza la Benin baada ya mahakama kuamuru wanyongwe
siku ya Jumatatu.
Alisema kesi zote za rufaa, hazikuweza kufua
dafu na hukumu zao tayari zikuwa zimetiwa saini -mbili na magavana wa
Edo Governor Adams Oshiomhole, huku nyingine zikitiwa saini na magavana
wa majimbo mengine.
Ikiwa itathibitishwa , hatua hii ya kunyongwa ni ishara ya kurejea kwa sheria kali ya hukumu ya kunyongwa nchini Nigeria.
Wahudumu wa magereza ndio waliotekeleza hukumu ya kunyongwa , kitengo cha serikali wala sio jimbo la Edo.
Kulikuwa na ripoti za kutatanisha kuhusu hali ya mfungwa wa tano.
Chino Obiagwu wa kitengo cha sheria na mradi wa kuwasaidia wafungwa hao alisema kuwa mwanaume huyo alinyongwa.
Hukumu ilicheleweshwa kwa muda kwa sababu za
kiufundi lakini baadaye wakapashwa habari kwa njia ya barua pepe,
alisema bwana Obiagwu.
Lakini bwana Idahagbon alisema mwanaume huyo hakunyongwa kwa sababu hukumu yake ilisema kuwa auawe kwa kupigwa risasi.
Hata hivyo shirika la Amnesty International
limesema kuwa limepokea habari zinazoweza kuthibitisha kuwa wafungwa
wanne walinyongwa mjini Benin.
0 comments:
Post a Comment