-Asema adhabu ya kadi nyekundu haikuwa na ulazima
-Asema wangecheza 11 ushindi ulikuwa wazi
Wachezaji wa Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Jumatatu alfajiri wakitokea Morocco.
Akitoa
maoni ya mchezo huo, Poulsen alisema alisikitishwa na jinsi refa huyo
alitoa adhabu kali ambayo haiendani na kanuni za FIFA.
Aggrey
Morris alioneshwa kadi nyekundu baada ya kugongana na Abderazak Hemed
Allah ambaye aliifungia Morocco bao la kwanza katika dakika ya 37.
“Hakuwa na sababu ya kumuonesha Morris kadi nyekundu kwani tayari alishawapa Morocco penalti, alisema Poulsen huku akiongeza, “FIFA imeshawaonya marefa mara kadhaa dhidi ya kuua mchezo kwa namna hii ya kutoa adhabu kali kupita kiasi.”
Poulsen
alisifu wachezaji wake na kusema licha ya kucheza pungufu walipambana
uwanjani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa Amri Kyemba. Morocco
walishinda kwa 2-1.
“Kama
tungecheza kumi na moja hadi mwisho nina uhakika tungeshinda mechi hii
lakini refa aliiua mechi na huwezi kufanya hivi katika mechi ngumu kama
hii,” alisema Poulsen.
Kocha
huyo alisema kupata goli la ugenini unapocheza na timu ngumu kama
Morocco ni jambo la kujivunia hasa mnapokuwa pungufu uwanjani.
Alisisitiza kuwa sasa wanaelekeza nguvu zote katika mechi shidi ya Ivory Coast Jumapili ijayo. “Mambo ya Morocco yamekwisha sasa tunafikiria namna ya kushinda mechi ya Jumapili.
Tanzania iko katika kundi C inayoongozwa na Ivory Coast yenye pointi 10, Tanzania 6, Morocco 5 na Gambia 1.
Taifa
Stars imerejea Jumatatu alfajiri kutokea Marrakech Morocco na
itaendelea na kambi ya wiki moja ili kujiandaa na mechi dhidi ya Ivory
Coast.
Nahodha
wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wachezaji walicheza kwa ari kubwa
na walifurahishwa na jinsi watanzania walijitokeza kwa wingi.
“Tulipata faraja kubwa sana kuwaona watanzania wengi uwanjani…mambo ya Morocco yameisha sasa tuangalie Ivory Coast,” alisema.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe ambaye bia yake
inadhamini Taifa Stars, alisema wachezaji walijitahidi hasa ikizingatiwa
walicheza pungufu na hata wakafanikiwa kufunga bao moja.
“Katika
hali kawaida, wachezaji wengine wangekata tamaa lakini bao hili moja
linaonesha kuwa wachezaji walikuwa na ari ya kupata ushindi,” alisema Bw Kavishe.
Alisema
wao kama wadhamini wana imani kubwa na Taifa Stars na kwamba wanaamini
hii ni safari ya mafanikio ambayo ilianza mwaka mmoja uliopita tangu Bia
ya Kilimanjaro Premium Lager ianze udhamini huo.
0 comments:
Post a Comment