Rais Barack Obama wa Marekani ameidhinisha uamuzi wa nchi yake kuwapa silaha waasi wa Syria kwa mara ya kwanza.
Uamuzi
huu unakuja masaa machache, baada ya Ikulu ya Marekani kutamka kwamba ina
ushahidi kamili wa utawala wa Rais Bashar al-Assad kutumia silaha za kemikali
dhidi ya waasi. Ikulu hiyo imesema kuwa, sasa Marekani itatoa msaada wa moja
kwa moja kwa upinzani wa Syria
huku chanzo kimoja cha serikali ya Marekani kikisema kuwa msaada huo
utajumuisha silaha na risasi. Uamuzi wa Marekani unafikiwa katika wakati ambapo
wanajeshi wa Assad, wakisaidiwa na Hizbullah, wanasonga mbele kuelekea ngome ya
wapinzani ya Aleppo.
0 comments:
Post a Comment