Duru za karibu na ikulu ya White House nchini Marekani zinasema
kuwa, mazungumzo ya siri yanaendelea kati ya Rais Barack Obama na
makamanda wake wa jeshi ili kutafuta njia ya kuweka marufuku ya kutopaa
ndege nchini Syria ili kulemaza nguvu za kijeshi za Rais Bashar Asad
dhidi ya wapinzani wake. Habari zinasema kuwa Marekani huenda ikakosa
kupata uungaji mkono katika Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala hilo kwa
kuzingatia kwamba Russia ina kura ya veto na inaweza kupinga jaribio
lolote la kuibana serikali ya Damascus. Inasemekana kwamba Marekani
huenda ikatumia kifua kuweka marufuku hiyo sambamba na kuwapa silaha
nzito magaidi wanaotaka kuipindua serikali halali ya Rais Asad. Hata
hivyo, Syria imesema iko tayari kukabiliana na mtu yeyote mwenye nia ya
kuharibu zaidi mgogoro wa nchi hiyo. Umoja wa Mataifa na Russia pia
zinapinga mpango wowote wa kutumiwa nguvu za kijeshi kutatua mgogoro wa
Syria.
Saturday, 15 June 2013
HOME »
» USA YAPANGA KUWEKA MARUFUKU YA KUPAA NDEGE SYRIA
0 comments:
Post a Comment