Mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na
Ivory Coast (The Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh.
502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi
za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh.
15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo
wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh.
7,809,104.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35
na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.
Asilimia
60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni
asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.
Mechi
iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo
iliingiza sh. 226,546,000.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF)
0 comments:
Post a Comment