Kocha wa Taifa Stars,
Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa
mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani
(CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi jana (Juni 17
mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa
dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa juzi (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Kim
amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa
isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.
Wachezaji
hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa,
Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto,
Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon
Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni
Chanongo na Zahoro Pazi.
Mechi
hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati
ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili
baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.
0 comments:
Post a Comment