Mwanasheria
Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Mark Bomani, amevitaka vyombo vya ulinzi na
usalama vya nchi hiyo kufuata misingi ya sheria katika utendaji wao wa kazi.
Jaji Bomani amevitaka pia
vyombo vya usalama vya Tanzania kuzingatia sheria katika matumizi ya silaha
kwenye matukio mbalimbali wanayokabiliana nayo.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa
Kongamano la Maadili ya Waandishi wa Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam
likiwa na kaulimbiu ya 'Wajibu wa Vyombo vya Habari Kupambana na Kauli za Chuki
na Itikadi Kali.'
Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Tanzania ameongeza kuwa, kumekuwa
na tabia ya baadhi ya vyombo vya dola kuwapiga watu bila kufuata sheria ambazo
zinakataza kufanya hivyo, lakini mambo hayo yanatokana na uelewa mdogo.
Amesema, hata maandamano na mikutano yoyote inapozuiwa pia ni lazima
vigezo na sheria zifuatwe ili kila mmoja au kinachofanyika kimezingatia sheria
na si uonevu au upendeleo.
0 comments:
Post a Comment