SOPHIA SIMBA
SERIKALI imesema inaangalia utaratibu wa
kufuta adhabu ya viboko shuleni ili kuweza kufanya mazingira ya shule
kuwa ni kimbilio kwa mtoto, badala ya kuwa tishio.
Wakati kauli hiyo ikitolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Zuberi Samataba, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba ametaka watoto wanaozaliwa magerezani wasifanywe kama wafungwa, bali wapatiwe haki zao za kimsingi ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu.
Simba alisema hayo Jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza katika mkutano wa kujadili utafiti uliofanywa juu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Alisema suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto bado ni tatizo na utafiti huo umeonesha ukatili unafanyika shuleni, nyumbani na maeneo mengine, unadhoofisha ukuaji wao wa kimwili na kiakili, bila kujali kama unafanywa na mwanafamilia au mtu mwingine ni ukiukwaji wa haki na misingi ya watoto.

0 comments:
Post a Comment