BAADHI ya wafanyakazi wa kampuni ya H/Young inayojenga barabara kisiwani
Pemba wanadaiwa kuwadhalilisha kimapenzi wafanyakazi wao wa kike na
kisha kuwapiga picha ambazo zinadaiwa kusambaa kwenye simu za mkononi.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia moja ya picha zinazodaiwa kusambazwa.
Hata hivyo, habari hizo zimekanushwa vikali na Mkuu wa Wilaya ya Wete
ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, Omar Khamis
Othman.
Mkuu wa wilaya hiyo amewataka wananchi kuacha kuipaka matope kampuni hiyo.
Alisema taarifa hizo hazina ukweli, kwani baada ya kufuatilia wameshindwa kubaini wahusika wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Wete, Mkuu huyo wa Wilaya
aliwataka wananchi walio na ushahidi juu ya picha hizo wapeleke ushahidi
wao ofisini kwake ili hatua zinazofaa zichukuliwe.
Alisema ofisi ya Wilaya imefanya ziara ya kuwatafuta wahusika wa vitendo
hivyo kutokana na picha hizo, lakini wameshindwa kupatikana kwani kila
sehemu walizokwenda walipelekwa sehemu nyingine.
"Mwanzo tuliambiwa anayedaiwa kudhalilishwa ni mkaazi wa Pandani, kufika
Pandani tukaambiwa kuwa ni mkaazi wa Piki, wakati wakaazi wa Piki wao
wakatuambia kuwa ni mkaazi wa Bopwe, na tulipofika Bopwe tukaambiwa
anaishi Kinyasini," alisema.
Aidha amewataka wananchi kuacha kuzua mambo ambayo hayana ushahidi wake,
kwani kitendo hicho kinawakosesha uwaminifu watendaji wa kampuni hiyo
katika jamii wanayofanya kazi
0 comments:
Post a Comment