Thursday, 13 June 2013

WABUNGE WASALIMU AMRI KWA KUDAI NYONGEZA YA MSHAHARA (KENYA)

Wabunge wa Kenya wamesalimu amri madai yao ya kuongezewa mshahara waliyokuwa wameshayapigia kura, lakini badala yake wakajiwekea posho kubwa zikiwemo gari za kifahari na mafao ya kustaafu, liliripoti shirika la habari la AFP siku ya Jumatano (tarehe 12 Juni).

Mwezi uliopita, wabunge wa Kenya walijipigia kura ya kupandisha mishahara yao, na kupindua makato yaliyokuwa yameamriwa na Kamisheni ya taifa ya Mishahara na Ujira (SRC).

Walipiga kura hiyo kupuuza amri za SRC na kukaidi maombi ya Rais Uhuru Kenyatta kwamba wawe na

uvumilivu, na kuongeza mshahara wao wa mwezi hadi shilingi 851,000 (dola 9,955).

Wanaharakati wamefanya maandamano ya aina hiyo nje ya jengo la bunge katika wiki za karibuni wakiwataka wabunge hao kukata malipo yao, ikiwemo maandamano moja ambapo waliachia nguruwe na
kumwaga damu ya wanyama.

Siku ya Jumanne, waandamanaji walicheza na nguruwe mkubwa wa karatasi na kupeperusha noti bandia na mabango yaliyoandikwa "MPigs".

Lakini SRC ilisema baada ya mazungumzo "yenye faida" na wabunge, wamekubali kuheshimu amri ya kukatwa kwa mshahara kwa takribani asiimia 40 hadi kufikia shilingi 532,000 (dola 6,222).

Wabunge walikubaliana na mpango huo baada ya kufikia muafaka juu ya ruzuku ya shilingi milioni 5 (dola 58,500) kwa ajili ya gari za kifahari. Ruzuku hiyo ilionekana kuwa 'jambo linalowezekana kuwa yenye mafanikio zaidi' kuliko kumpa kila mbunge gari na dereva wake kwa wabunge wote 416, ilisema SRC.

  SabahiOnline.com

 

0 comments: