Saturday, 15 June 2013

WAISLAMU UFARANSA WAANDAMANA NA KUPUNGA UBAGUZI


    Wapinzani wa ubaguzi dhidi ya dini ya Kiislamu nchini Ufaransa, wamefanya maandamano kulalamikia hatua za mara kwa mara za kibaguzi dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu nchini humo.

     Maandamano hayo makubwa ya kupinga ubaguzi huo wa kidini, yalifanyika katika mji wa Argenteuil ulioko kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Paris. Maandamano hayo yamefanyika kulalamikia mashambulizi ya wiki kadhaa zilizopita mjini hapo dhidi ya Waislamu. 

    Mkuu wa kamisheni ya kupambana na ubaguzi wa kidini (CRI) Abdul-Aziz Chaambi, amesema kuwa, mashambulizi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa, yanazidi kuchukua sura mpya huku serikali ya Paris ikishindwa kuchukua hatua zozote za kukabiliana na hali hiyo.

     Ameitaka serikali ya Ufaransa kuhakikisha inamaliza hali hiyo mara moja. Hivi karibuni jeshi la polisi nchini Ufaransa lililazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za plastiki kuwatawanya watu waliopandwa na hasira, baada ya askari polisi kumkamata mwanamke aliyevaa burqa ya Kiislamu pambizoni mwa Paris, mji mkuu wa nchi hiyo.

    Chanzo Iran swahili radio

    0 comments: