Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa
Pierre Mauroy amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84.
Habari
za kifo chake zimetangazwa leo hii na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa
Laurent Fabius.Mauroy ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 1981 na
mwaka 1984 chini ya Rais wa kwanza Msoshalisti nchini Ufaransa Francois
Mitterand alikuwa amefanyiwa upasuaji wa uvimbe wa satarani katika pafu lake
hapo mwezi wa Aprili. Rais Francois Hollande ambaye yuko katika ziara rasmi nchini
Japani amemuelezea Mauroy kuwa ni mtu aliyeitumikia Ufaransa wakati wa vipindi
vya aina yake ambapo alichukuwa hatua za kishujaa na kuitumikia nchi yake bila
kudhoofisha misingi yake muhimu. Mauroy alikuwa meya wa mji wa Lille kwa miaka 28 tokea mwaka 1973 hadi
mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment