Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Kebwe Kebwe amewataka viongozi wa halmashauri kushirikiana na waganga
wakuu kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinavyotolewa na Serikali kupitia
Bohara Kuu ya Dawa MSD vinatumika ipasavyo.
Dkt. Kebwe alisema hayo jana
wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara ya kwanza toka uteuzi wake
kutoka kwa Rais Kikwete wakati akiwa na kamati ya kudumu ya Bunge
huduma za jamii kukagua taratibu za usambazaji dawa vituo na hospitali
za Serikali.
Katika ziara hiyo amezitaka
Hospitali za Serikali kutumia vyanzo vingine vya mapato ili kuweza
kununua dawa na vifaa tiba katika kuongezea matumizi mbalimbali na
bajeti ya Serikali.
“ni muhimu kuelewa kuwa hospitali inavyanzo vingi vya mapato wakati umefika sasa kutumia fursa hizo katika kuhakikisha mapato yanayotokana na vyanzo vya hospitali yanatumika pia katika kuongeza ununuaji dawa na vifaa tiba ili kuipa uwezo Serikali na jamii kufikia huduma ipasavyo”alisema

Naye Mwenyekiti wa kamati ya
kudumu ya Bunge huduma za jamii Magreth Sita alisema ni muhimu suala la
upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kupewa kipaumbele cha hali ya juu
kutokana na kuwa ndio msingi wa huduma bora za afya kwa jamii.
Alisema kutokana na ufanisi
mkubwa uliopo katika upatikanaji dawa hospitalini na vituo vya afya
baada ya mfumo wa ufikishaji dawa moja kwa moja hadi vituoni (DD)
unaofanywa na MSD ni vizuri Serikali kutambua kuwa ufanikishaji wa hatua
hiyo unahitaji uwezeshi hasa wa fedha za bajeti kufika kwa wakati.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya
wadhamini MSD Dkt Ahmed Hingola alisema endapo Serikali itadhiti na
kuhakiki dawa chache zilizopo ili kutekeleza mahitaji ni wazi lawama za
wananchi kwa bohari ya dawa zitakwisha.
“MSD kazi yake kubwa ni upelekaji wa dawa huku usimamizi wa matumizi katika kutumika kama ilivyokusudiwa ikiwa bado ni changamoto hasa katika sehemu husika hivyo MSD imeanza harakati za uwekaji wa nembo dawa za Serikali (GoT) ili kudhibiti dawa hizo zisiweze kupita njia za panya”alisema

0 comments:
Post a Comment