Thursday, 6 February 2014

SEMINA YA USIMAMIZI WA UCHAGUZI WA KALENGA YAFUNGULIWA LEO KATIKA MANISPAA YA IRINGA

Semina ya mafunzo ya msimamizi mkuu na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata ya Kalenga imefunguliwa leo katika ukumbi wa Siasa ni kilimo katika Manispaa ya Iringa huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Dokta Leticia Warioba.

 
Akiongea mbele ya washiriki wa Semina hiyo Dokta Warioba alisema uchaguzi unakaribia kufanyika hivi karibuni hivyo amewataka wawe waaminifu na makini siku ya uchaguzi pia hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaekiuka sheria na taratibu za usimamizi wa uchaguzi.
 
Na kwa upande wa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Iringa Prudencia Kisaka aliitaja siku ya kutoa fomu za uteuzi ni kuanzia tarehe 9 mpaka tarehe 18 mwezi huu.
 
Pia amesema uteuzi wa vyama utaanza tarehe 18 mwezi huu ambapo kampeni za wagombea zitafanyika tarehe 19 februari mpaka tarehe 15 machi mwaka huu, hivyo siku ya upigaji kula itakuwa ni tarehe 16 machi ambapo daftari litakalotumika ni lilelile la mwaka 2010.
 
NA DIANA BISANGAO WA  , IRINGA

Related Posts:

0 comments: