Thursday, 6 February 2014

FISI WAFUKUA KABURI NA KULA MIILI YA WATU WALIOUAWA NA WANANCHI

 
 
 NA BUNDALA WILLIAM.   SHINYANGA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji cha Iponya kata ya Kagongwa Wilayani Kahama Mkoani Shinyinga wamelazimika kuzika upya mabaki ya Marehemu wawili waliozikwa wiki iliyopita baada ya leo kukuta wamefukuliwa na Fisi.

Miili hiyo ni ya watu wawili ambao walisadikiwa kuwa vibaka waliuwawa na wananchi wenye hasira kali na kuchomwa moto na kisha kuzikwa katika makaburi yaliyopo katika kijiji hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda wakizungumza mwandishi wetu wamesema hali hiyo imetokana na kuzikwa katika makaburi ambayo hayana kina kirefu hivyo wanyama hao kuwa rahisi kwao kufukua na kuanza kula maiti hizo....

Mmoja wa mashuhuda Hasan Msoma amesema waligundua kutokana na wao kufika katika maeneo ya makaburi kwa lengo la kuzika Mtoto ndipo wakaona mabaki ya miili ya marehemu huku eneo kubwa la miili ikiwa imeliwa na fisi.

Amesema baada ya kuona hali hiyo waliutaarifu uongozi wa kata ambao ulifika na kushiriki katika mazishi na kusema kuwa haki za binadamu hazikuzingatiwa katika kuzika watu hao kwani walifukiwa katika shimu lenye kina kifupi cha futi moja.

Hata hivyo viongozi wa kata hiyo hawakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kutokana na kutoonesha ushirikiano kwa mwandishi wetu.

Related Posts:

0 comments: